Afya ya Akili
Ni katika maadhimisho ya Afya ya Akili yaliyofanyika mnamo
katikati ya mwezi Machi mwaka huu katika hospitali ya
wilaya ya Hanang’, inayojulikana kwa jina la Tumaini, ambapo mkuu wa
wilaya ya Hanang, Mh. Luteni Ligubi aliwahusia wananchi wa wilaya hiyo ya
Hanang’ juu ya umuhimu wa afya ya akili.
![]() |
| Mh. Ltn Ligubi, Picha na Goustone Isole |
ishwa kutokana na kuwepo kwa barabara yenye ubora wa kiwango cha lami inayotazamiwa kukamilika ujenzi wake katikati ya mwezi Mei mwaka huu hivyo uingizaji wa haramu wa madawa ya kulevya utakuwa ni jambo lisilozuilika kama wananchi hawatatoa ushirikiano wa kutosha hususani kwa chombo cha usalama, jeshi la polisi.
![]() |
| Kikundi cha sanaa, Katesh |
Mkuu huyo wa wilaya alitoa hamasa kwa waratibu wa afya ya
akili katika hospitali hiyo ya wilaya kuandaa matamasha yanayokusudia
kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa afya ya akili. Akizungumza kama mgeni wa
rasmi, Mh. Luteni Ligubi alitanabanisha kwamba madhara yatokanayo na uharibifu
wa afya ya akili ni pamoja na kuongezeka kwa matukio ya uhalifu katika jamii,
wimbi la umaskini katika ngazi zote kuanzia familia hadi Taifa pamoja na
maambukizi ya magonjwa hususani yale ya zinaa.
Aidha mkuu huyo wa wilaya alichukua nafasi hiyo pia
kukichangia kikundi cha sanaa ya maigizo na nyimbo kinachojulikana kama ‘Upendo
Group’ kiasi cha pesa taslimu shilingi laki moja ikiwa ni kama sehemu ya
mchangokutoka ofisi yake ili kukiendeleza kikundi hicho ambacho pia kilikuwa
kikihamasisha wananchi wakati wa tamasha hilo.
Naye mratibu mratibu wa afya ya akili katika hospitali hiyo,
Bw. Tluway, alitamka kuwa idara yake itakuwa ikiandaa matamasha ya mara kwa
mara katika mikusanyiko ya watu kwa ajili ya kuhamasisha afya ya akili.
Tumia mawasiliano yanayoonekana kwenye kurasa tofauti na hii ndani ya Blog.



No comments:
Post a Comment