Na Goustone Isole
Hifadhi za Taifa Tanzania
![]() |
| Ramani ya Tanzania |
Tanzania ni moja
kati ya nchi tano zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchi hii ipo upande
wa Mashariki kabisa mwa bara la pili kwa ukubwa duniani baada ya lile la Asia,
Afrika. Nchi hii kwa upande wa Mashariki imepakana na bahari ya Hindi.
![]() |
| Mlima Kilimanjaro |
Nchi ya Tanzania
inasifika ulimwenguni kutokana na vivutio vingi, vikijumuisha vya asili na
kihistoria. Vivutio vya asili ni vile ambavyo vimekuwapo tangu enzi na enzi kwa
mfano mbuga za wanyama, milima na maziwa makubwa. Tanzania inasifika kwa kuwa
na mbuga kubwa za wanyama wa porini kama vile Serengeti na Ngorongoro. Kwa
upande wa milima, kuna mlima Kilimanjaro, Mlima mrefu kuliko yote barani
Afrika, upatikanao mkoa wa Kilimanjaro uliopo karibu na uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kilimanjaro, Kilimanjaro International Airport (KIA). Pia kuna milima ya
Usambara, Mlima Meru na mengine mingi ambayo pia makazi ya wanyama wa porini
pamoja na ndege wa aina mbalimbali. Maziwa maarufu yapatikanayo nchini Tanzania
ni Ziwa Victoria, ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, ziwa Tanganyika, ziwa
lenye kina kirefu kuliko yote barani Afrika bila kusahau ziwa Nyasa.
![]() |
| Simba akiwa mbugani, Serengeti |
![]() |
| Kondoa- Irangi |
Tanzania na Utalii
Nchi ya Tanzania
imekuwa ikifaidika kutokana na vivutio vya utalii. Kila mwaka idadi ya watalii
kutoka sehemu mbalimbali duniani imekuwa ikifika nchini Tanzania kujionea
vivutio hivi pamoja na maajabu yanayopatikana katika nchi hii. Mojawapo kati ya
maajabu ambalo limekuwa likijipatia umaarufu kila kukicha ni ile hali ya
wanyama wa mwituni kuishi pamoja na binadamu katika hifadhi ya Ngorongoro.
Uwepo wa watalii ndani ya Tanzania umesaidia sana upatikanaji wa fedha za
kigeni na pia umekuwa chachu ya nchi hii kutambulika kimataifa.
![]() |
| Hotel ya Kitalii |
Utalii pia umechangia
maendeleo ya sekta nyingine kama vile usafirishaji na biashara kwani kumekuwepo
ujenzi wa barabara katika viwango vya lami hasa katika maeneo yenye vivutio vya
kitalii, ujenzi wa mahoteli makubwa kama ilivyo katika mji wa kitalii, Arusha,
maarufu kama Geneva ya Afrika.
Ni jambo la
msingi kwa watanzania kuvilinda na kuviheshimu vivutio hivi kwani vimekuwa
msaada mkubwa hasa katika suala la maendeleo. Kutokana na pesa zinazotokana na
utalii, nchi ya Tanzania imeweza kufanya mambo ya kimaendeleo kama vile nilivyoonesha
hapo awali na pia imesaidia ujenzi wa mashule na pia hospitali karibu kwa kila
kata nchi nzima.
Hali ya Utalii wa Ndani nchini Tanzania (Domestic Tourism)
Utalii wa ndani
katika nchi ya Tanzania umekuwa si wa kuridhisha japokuwa kumekuwepo hamasa
kutoka kwa mamlaka ya hifadhi za Tanzania maarufu kama Tanapa. Hamasa hizi ni kama vile kuwatoza wazawa fedha kidogo. Hii bado
haijasaidia kushinikiza utalii wa ndani. Ni wazi wengi wa watanzania hawajafahamu
nini maana ya utalii na cha ajabu ni kwamba hawajachukua hata nafasi ya
kujiuliza ni kwa nini wageni kutoka nje hufika nchini mwetu kuja kushuhudia
vivutio hivi.
![]() |
| Watalii wa Nje |
Ni wazi sasa
baada ya kuyasoma yote hapo juu, utahamasika na kufikiria kutembelea moja ama
baadhi ya hifadhi zipatikanazo hapa nchini Tanzania na pia kushiriki vyema
katika kuhakikisha tunazihadhi ipasavyo hifadhi zetu.
Kufahamu hifadhi
zipatikanazo nchini Tanzania, bonyeza hapa.
Kufahamu jinsi Shirika la hifadhi za Taifa linavyofanya kazi na jinsi ya kutembelea mbuga za wanyama pamoja na vivutio vingine, Bonyeza hapa ku-download **('PDF' file in English (UK)**.
Kurudi juu, bonyeza hapa
Kufahamu jinsi Shirika la hifadhi za Taifa linavyofanya kazi na jinsi ya kutembelea mbuga za wanyama pamoja na vivutio vingine, Bonyeza hapa ku-download **('PDF' file in English (UK)**.
Kurudi juu, bonyeza hapa






No comments:
Post a Comment