Saturday, March 24, 2012

Katesh sekondari hali si shwari!!


Mwandishi wa Blog hii, Goustone
Ni majuzi tu tangu Baraza la Mitihani Tanzania, maarufu midomoni mwa wengi kama Necta,  litangaze matokeo ya kidato cha nne mwaka 2011 na kuonekana kwamba ufaulu kwa kiasi kikubwa umeshuka isivyo kawaida..... Kutokana na hilo hofu na mashaka imekuwa ikitanda miongoni mwa wazazi na hata wanafunzi pia juu ya maisha yao ya baadaye ikizingatiwa wengi wetu tunatoka katika familia maskini tukitegemea Elimu kuwa mkombozi wa maisha ya kesho..

Tutegemee wenzetu wasomao St. Mary's na St. Thomas wafaulu na si wao wa St. Kayumba ambao hata kipande cha muhogo kabla ya kuanza masomo ya siku ni hadithi ya Bulicheka na tufani baharini isiyo na mwisho na hata mwisho wake tunautamani uendelee....

Kwa kulitambua hilo kuwa wao wa St. Kayumba msingi wao wa maisha ni Elimu, zimeibuka tafrani nyingi kati ya nyongozi za shule na wanafunzi... kumbuka kule Tabora... mpaka viongozi baadhi wakahamishwa.. eti wengine wakapandishwa vyeo baada ya kubadilishwa vituo vya kazi!! Hii inasikitisha..... eti mchafu ghafla ghafla anapakwa mafuta na kisha kusindikiza maharusi kuelekea jukwaani angali walio nadhifu na kunukia marashi ya Zanzibari wanaachwa nyuma... Serikali ya Tanzania inapaswa kuwa makini na hili...

Tuachane na hayo... turudi kwetu Manyara, mkoa unapopatikana Mlima mrefu wa Hanang' ushikao nafasi ya nne kwa urefu hapa kwetu Tanzania...
Eti mkuu wa shule fulani nilioitaja hapo juu kwenye 'title' anang'ang'ania shule angali inaonekana dhahiri hawezi kumudu uongozi.... Hii imepelekea tafrani baina ya Mkuu huyo ambayo nimeonelea si jambo jema kulianika jina lake hapa kwa kuhofia lisije likakauka na kupoteza utamu wake!!!

Wanafunzi wanadai mkuu huyo amekuwa chanzo cha kushuka kwa taaluma shuleni hapo ukilinganisha na miaka ya nyuma.... ni hofu ya wanafunzi yaliyotokea mwaka jana kidato cha nne yakatokea na mwaka huu 2012... Kwa takwimu inaonekana shule hiyo imekuwa ikifaulisha kwa kiwango kizuri hata cha daraja la kwanza, lakini kwa mwaka jana hata daraja la pili ilikuwa ni ndoto ambayo haina mwanzo wala mwisho...

Cha kusikitisha, wanafunzi wamejaribu hata kujichukulia hatua ya kutaka kumtoa madarakani mkuu huyo wa shule kwa madai kuwa anaharibu shule hiyo na hivyo si budi aachie ngazi... Zaidi wanataka na hata huduma kama za msosi ziboreshwe kwa kuwapa sare nyeupe wapishi.. na ikitokea sare ya mpishi ikawa na hata doa la jivu basi aeleze ni kwa nini imekuwa hivyo!!!, kingine ambalo hata mimi nimeona ni la msingi ni wao kudai madarasa kuwekewa Ceiling Board kwani kumekuwa na Voice Interference wakati wa masomo kati ya madarasa yanayoungana, mbaya zaidi ukute ni form one na kidato cha pili.
Kibaya zaidi wakadiriki hata kuharibu mali ya shule kwa kuvunja madirisha ya vioo.... Jamani wanafunzi hata ikiwa mnadai haki zenu tumieni busara!!!!



HAKI ELIMU

No comments:

Pageviews past week