Na Goustone Isole
Kila kukicha mapenzi katika maisha ya mwanadamu yamekuwa
yakichukua nafasi kubwa ukiacha suala la kutafuta hela au mambo mengine
yahusianayo na maendeleo.
Kutokana na hilo, nachukua nafasi hii, mimi kama mmoja wa
wakereketwa wa suala la mapenzi, kuelezea kwa undani mambo muhimu ya kuzingatia
katika mahusiano.
![]() |
| Wapenzi wenye furaha |
Imekuwa ni kwa kawaida kwa mtu yeyote kusikika akisema eti
mapenzi ya kweli hayaangalii pesa au mali…. hii naikataa tena kwa asilimia
zote!! Kwa utafiti mdogo nilioufanya kwa muda usiopungua miaka minne… nimegundua kwamba wengi wanaojinadi kuwa
mapenzi hayaangalii kipato ni wale ambao hujiingiza kwenye mahusiano na wapenzi
zaidi ya mmoja… hii ikimaanisha kuwa
mmoja/ wengineo ni wa kujipatia kipato na mwingine ni wa kuridhisha moyo wake
kwa kuwa ndiye anayempenda kwa moyo wake wote ila kwa sababu ya yeye kuwa na
kipato kidogo basi anakuwa hana budi kufanya kile ambacho kitamsaidia katika
dunia hii ya Sayansi na Teknolojia. Hii pia hutokea kwa wanaume wapenda vya
bure.
Ukweli ni kwamba hakuna binadamu yeyote apendaye maisha
mabaya….. na tutambue katika maisha yetu ya kila siku tangu enzi na enzi tena
zile za Adam na Hawa, mwanaume aliumbwa mtafutaji na mwamuzi wa mambo mengi
katika maisha ya kila siku iwe ni katika nyanja ya kijamii, kiuchumi au hata
kisiasa. Cha ajabu kutokana na utandawazi
basi siku hizi wanawake na wao wanajiweka mstari wa mbele kudai haki ya kuwa na
maamuzi katika nyanja zote zilizozibainisha hapo awali. Kama matokeo yake, leo
si ajabu kuona mwanamke ameoa mwanaume, na yeye mwanamke kuwajibika kwa kila
hali kuhakikisha mwanaume anafurahi kama ambavyo wanaume wengi wapendavyo
kuhakikisha wanawafurahisha wapenzi wao
kwa kuwapa yale wanayohisi ni bora zaidi… Mbaya zaidi ikitokea kwamba mwanaume
akashindwa kumfurahisha mpenzi wake ni kawaida kwa mwanaume kuleta visingizo
vya hapa na pale ili mradi tu aachane na mwenzi wake yote ili kuepusha fedheha
ya kushindwa kuonesha udume wake!!! Kwa mfano huo hafifu nadhani ntakuwa
nimeeleweka kuwa Mahusiano na Uwezo ni vitu ambavyo vinaenda kwa pamoja….
![]() |
| Wapenzi wakijadiliana jambo |
Wachangia mada waliweka bayana kwa kuonesha kuwa ni rahisi
kwa mwanaume kukubalika kwa upande wa binti kama tu atakuwa na mambo yafuatayo
- · Elimu ya kutosha angalau hata Shahada moja ikiwa ni imani ya wazazi kuwa mwanaume mwenye Elimu ana uelewa mpana na hivyo inakuwa ni rahisi katika suala zima la kupambana na maisha.
- · Pia ni imani kuwa huwa ni sifa kwa wazazi wa binti kuona binti yao ameolewa na watu wafanyao kazi za sifa kubwa kama vile Madaktari au wanasheria.
Pamoja na kuweka hoja hii wazi, sijamaanisha eti wazazi basi
wawachagulie mabinti zao au hata vijana wao wenza … Hiyo sitaki kusikia hata
kidogo!! Vijana mna haki katika masuala ya mahusiano katika kuchagua mwenza,
nafasi ya mzazi au mlezi ni kushauri tu na kufundisha namna ya kuishi maisha ya
wawili (Ndoa).
Niwatakie maisha mema vijana wa leo au wazee wa kesho hasa
ya Mahusiano….
Wenu katika Kuelimishana, Kaka Goustone Isole


No comments:
Post a Comment