Friday, March 23, 2012

Hawa ni Hatari....!!!


Ni aibu……..

Ni majuzi tu maeneo ya Qedang'onyi ndani ya mji mdogo wa Katesh mkoani Manyara ambapo vijana wawili wa kike ambao majina yao hayakuweza kupatikana mpaka naondoka eneo la tukio walipotia fora baada ya kukamatwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba nguo za Bi. Selina Paulo, mkazi wa eneo la Qedang'onyi, zilizokuwa zimeanikwa kwenye kamba baada ya kufuliwa.

Wezi hawa katika pozi baada ya kukamatwa
Hata baada ya kukamatwa, vijana hao walionekana kutokuwa na wasiwasi wowote kiasi kwamba walikuwa wakichekelea jicho la kamera yangu kama wanavyoonekana katika picha upande juu kushoto.... Baada ya kuwatia mikononi wezi hao, Bi. Selina Paulo alichukua hatua ya kuwauliza vijana hao ni wapi walipokuwa wamepeleka nguo hizo na wao kujibu kuwa sio wao waliokuwa wamechukua!! Majibu hayo yalimfanya Bi. Selina kuchukua hatua mkononi kwa kuwagonga makwenzi ya kutosha na vijana hao kujikuta wakikubali kuwa wao ndo wahusika wa wizi huo wa nguo.. Iliwalizimu kuonesha ni wapi ambapo walikuwa wamehifadhi nguo hizo...

Kwa mujibu wa wezi, wanasema hatua ya kuwa wezi ni baada ya maisha kuwa magumu kwa kukosa kipato kinachowawezesha kuyamudu maisha.
Kutokana na tukio hili, washukiwa (wezi) baada ya kukamatwa na kutoa maelezo kuhusiana na sababu iliyowapelekea wao kufanya hivyo, waliomba kwa wanajamii msaada wa kuweza kupata ajira yoyote ili kuweza kuyamudu maisha na hivyo kuepukana na matendo ambayo ni kinyume na maadili ya jamii. Aidha mabinti hao waliongeza kuwa wamekuwa wakijihusiha na biashara ya ukahaba ikiwa ni sehemu ya kutafuta mlo wa siku.

Taarifa hii imeandaliwa na
Goustone Francis Isole  +255 754 924 738, +255 788 298 096, +255 654 596 502



No comments:

Pageviews past week