![]() |
| Baraza la Mitihani |
Leo sina mengi ila napenda tu niwausie jambo moja ambalo nimeanza kwa kulionesha kwenye 'title' hapo juu..... si lingine ni kuhusiana na Elimu!!!
Kumekuwa na mambo mengi yasemwayo kuonesha upana wa Elimu hii hususani ambayo wazungu wanaiita 'Formal Education'... Ukienda shule fulani utasikia... Elimu ni Bahari, mara Elimu ni Ufunguo wa Maisha... hiyo ni baadhi tu ya misemo inayolenga kuonesha Umuhimu wa Elimu katika Maisha.... Kwa Kulitambua hilo serikali ya Tanzania iliamua kuanzisha kitengo kitakachosimamia masuala yahusiyo Elimu hasa katika michakato mizima ihusianayo na Mitihani.... Hicho si kingine ni Baraza la Mitihani Tanzania.. Zaidi ya hapo kumekuwepo na Wizara maalumu ya kusimamia mambo ya Elimu kwa ujumla.... hiyo si ingine ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi!!!
Kutokana na hilo ninapenda kuwaambieni kuwa Serikali yetu inawapenda sana watanzania... na nafasi tunazopewa na nchi yetu, basi tuzitumie!! Na pia ni ukweli usiopingika kuwa bila Elimu... huwezi fanya lolote katika maisha!!
Kuonesha kwamba unajali sana Elimu na hukufanikiwa kupata Elimu ya Sekondari au uliipata angalau ya kufikia kidato cha nne na hukufaulu vizuri na unatakaka kurudia mitihani hiyo Bonyeza hapa.
- Kuangalia matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE 2011) Bonyeza hapa.
- Kuangalia matokeo ya mtihani wa Maarifa (Qualifying Test 2011) Bonyeza hapa.
francis.goustone88@aol.com

No comments:
Post a Comment