Sunday, March 23, 2014

Yataisha lini?!!!!!

Mwandishi, Bw. Goustone Isole

Imeandikwa na Goustone Isole. St. Augustine University of Tanzania- Mwanza. 


Tunapoelekea sasa sijui ni wapi? Suala la kujichukulia hatua za kisheria mkononi (mob justice) kwa kweli limezidi kushika makucha yake. Ni majuzi tu, usiku majira ya 3: 45 tarehe 21 Machi, 2014 maeneo ya Kwa Masha (Malimbe- Nyegezi) ndani ya eneo lililopo nje kidogo ya mji wa mwanza ambapo kijana mmoja (Jina halikuwa limefahamika mpaka habari hii inaandikwa) anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 26-29 alipouawa kikatili kwa kukatwakatwa na
 


Kijana huyo akiwa amepoteza maisha muda mfupi baada ya kupata kipigo kutoka kwa wanachuo... picha na Goustone Isole




mapanga mwili mzima na sehemu ya upande wa kushoto mwa kifua kutobolewa. 
Si hapo tu, sehemu ya mabega inayounganisha mikono yote miwili ilikatwa na kubaki ikining’ia.
Ilikuwaje?
Kwa wadodosaji walioshuhudia tukio hilo mwanzo mpaka mwisho walilielezea tukio hilo kama ifuatavyo:
Ilikuwa ni majira ya 11 jioni kijana huyo aliyekuwa anaonekana mtanashati alipofika hostel fulani inayojulikana kwa jina Junior iliyopo hapa SAUT- Malimbe kwa madai kuwa amekwenda kumtembelea rafiki yake mwanachuo, hii ni kwa madai ya mlinzi wa hostel hiyo. Baada ya kuingia ndani haikuchukua muda kulisikika sauti ya msichana ikipiga kelele kwamba kuna mwizi. Na hapo ndipo vijana wa kiume wa hostel ile na za jirani walipofika na kumtia nguvuni kijana huyo na kumpeleka kwenye chumba kwa ajili ya mahojiano. Katika mahojiano hayo ilionekana marehemu alikuwa ameagizwa na mwenzake anayepatikana maeneo ya Nyahingi kwenda kufanya ‘survey’ ili baadaye waweze kufanya tukio la wizi hostelini hapo.
Siku hiyo bahati haikuwa kwao kwani kijana huyo aliishia mikononi mwa vijana hao waliokuwa na hasira kali kufuatia matukio ya wizi hasa ya simu na laptops yalioshika kasi katika maeneo ya hosteli za wanachuo karibu na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino.
Hata polisi na mwenyekiti wa mtaa walipofika eneo hilo hawakuweza kukabidhiwa mtuhumiwa ambaye sasa ni marehemu kwa madai kwamba wezi wanapokabidhiwa kwao (polisi) baada ya muda mfupi huachiwa huru na kuonekana tena mitaani hivyo huyo walipaswa kumwajibisha wao wenyewe.
Ni baada ya polisi kuondoka maeneo hayo ambapo mtuhumiwa alitolewa nje majira ya 3 usiku na kuanza kupigwa kwa sime na majambia mpaka kupoteza maisha pale pale.

NINI KIFANYIKE KUZUIA WANACHI KUACHA KUJICHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MIKONONI?


Sio kweli kwamba wananchi wanapenda kujichukulia sheria mikononi, la hasha! Ni utendaji mbovu wa jeshi la polisi wanaouonesha pindi wanapokabidhiwa wahalifu. Hivyo ni vyema polisi wakawajibika ipasavyo ili kuzuia matendo kama haya ya kujichukulia sheria mkononi!

1 comment:

Anonymous said...

Inasikitisha sana

Pageviews past week