Sunday, April 29, 2012

Mh. Mary Nagu ni mfano wa Kuigwa!!

 Imeandikwa na Goustone Isole
Mh. Mary M. Nagu
Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya viongozi wetu nchini na hata katika nchi nyingine kujinadi mbele ya wananchi hususani kwa kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake unakuwa si wa uhakika.
Ninapomzungumzia Mh. Mary Michael Nagu, Waziri wa Nchi Uwezeshaji na Uwekezaji, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Hanang, ni watanzania wengi wataniunga mkono kwamba amekuwa kiongozi imara asiye tetereka hasa katika suala la utekelezaji wa ahadi azitoazo kwa wananchi.
Kwa wananchi wa Hanang, hii hadithi kwao ni dhahiri imeonekana tangu, Mama yao huyo alipolishika jimbo hilo…. Amefanya mengi, ikiwamo ujenzi
 
wa hospital ya kata Endasak ambayo imekuwa ikisaidia wananchi kutoka kata zilizo karibu na hiyo ya Endasak, kwa mama zetu hiyo imekuwa ni faraja kubwa ukizingatia ilikuwa ni taabu kwa wao kusafiri mwendo mrefu hadi katika mji wa Katesh ili kupata huduma…. 


Kwa kweli ilikuwa hatari, kwani mama zetu wengine walijifungulia njiani wengine hata kufariki kwani hata usafiri tu ulikuwa ni shida na hata kama haukuwa wa shida, na barabara je!! Leo Hanang unasafiri kwa raha kwani ujenzi wa barabara kwa kiwango cha ulami ndio uko njiani kukamilika kutokea  Arusha mpaka Singida na hata mpaka mikoa mingine kama Tabora mpaka Mwanza na kwingineko. Hapo wana Hanang’ wanapaswa sana kumshukuru mama yao!!! Hakuushia hapo katika suala la afya…. Alihakikisha hata hospitali ya wilaya al-maarufu kama Tumaini inatoa huduma bora!!! Suala la maji pia ni moja kati ya mambo aliyotilia mkazo!! Leo hii Hanang ya siku ile haipo tena!!
Hapa akiwa na wanafunzi, Gidahababieg




Tuingie katika lengo baada ya sifa zote kum mwagia mama M. Nagu, ni mnamo tarehe 4 mwezi wa Februari mwaka wa 2012, ambapo mama Mary M. Nagu akiambatana na viongozi wengine wa C.C.M ngazi ya kata na hata wilaya alipotembelea Hanang… Alikuwa na lengo moja tu, hili lilikuwa kuwajulia hali wananchi wake na pia kuwasikiliza mapungufu yao ili awapo ndani ya vikao vya bunge aweze kuyawasilisha. Pamoja na hayo alipata fursa ya kufungua ofisi ya kijiji kinachojulikana kama Gidahababieg. Kwa sababu ofisi hii haikuwa imepalizwa, basi Mama Nagu hakusita kabisa kunyoosha mkonowake  ili kuwezesha ununuzi wa mabati ili kukamilisha  ujenzi wa ofisi hiyo ambayo ilikuwa ni matunda ya nguvu za wananchi wenyewe. Yeye kama kiongozi wa jimbo hilo la Hanang pia alipata fursa ya kuzungumza na viongozi wa kitongoji hicho cha Gidahababieg wanaosimamia masuala ya misiba ambapo waliomba msaada wa masufuria makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika matukio ya nayohusiana na misiba. Hapo mama Nagu pia hakusita , aliahidi kutoa sufuria moja  kubwa kwa ajili ya kila kitongoji ambavyo kwa ujumla vipo tisa.
Hapa akifungua mchezo wa siku kiwanjani , Gidahababieg
Hakuishia hapo Mary Nagu, alipata pia nafasi ya kutembelea shule ya sekondari Gidahababieg ambapo pia alipata fursa ya kutembelea mazingira yake na kuahidi kuongeza idadi ya nyumba za walimu na kuziboresha zilizopo kwa kuleta umeme na maji ili kuhamasisha walimu kutenda kazi kwa bidii.
Mh. Mary M. Nagu pia alihamasisha pia michezo miongoni mwa wanafunzi wa shule ya sekondari Gidahababieg kwa kuwapatia mipira kwa ajili ya michezo ya mpira wa miguu na wa pete.
Mwisho kabisa Mh. Mary M. Nagu alijumuika na wananchi katika tafrija ndogo iliyoandaliwa na wananchi hao na baadaye kuagana nao.
Taarifa hii imeandaliwa na mwandishi wa habari wa kujitegemea, Bw. Goustone Isole




Pageviews past week